Sababu Moja Kwanini Hausongi Mbele Pamoja Na Juhudi unazoweka.

Image result for limitations
Umekuwa ukihangaika sana na kupambana vilivyo katika kutaka kuhakikisha kuwa unafanikiwa na unakuwa mwenye maisha bora au mafanikio ambayo unayataka, lakini pamoja na juhudi nyingi ambazo umekuwa ukiweka bado umekuwa ukijikuta hausongi mbele hata kidogo. Jambo hili laweza kusababishwa na vitu vingi sana lakini hapa nataka kukueleza kwa ufupi sana jambo moja tu ambalo linakufanya usisonge mbele, ambalo ni mipaka unayojiwekea katika akili yako na maisha kwa ujumla.

Binadamu kwa kawaida amekuwa ni mtu mwenye kujiwekea mipaka mingi sana katika akili yake, si semi kuwa ni vibaya kuweka mipaka katika akili yako lakini inategemeana na ni aina gani ya mipaka ambayo unajiwekea katika maisha yako. Kumbuka huwezi kufanikiwa kama mipaka unayojiwekea ni yenye kujaa wasiwasi, hofu na visingizio. Yaani akili yako hapa unakuwa umeiwekea mipaka kuwa inakuwa inafanya kazi kwa baadhi ya mambo na baadhi ya mambo inalala. Mipaka yaweza kuwa pia ni ile hali ambayo ukitaka kufanya kitu linakuja wazo la achana na hilo jambo achana na hilo jambo, na unaachana nalo bila kujiuliza kwanini uachane nalo.

Mipaka mingine yaweza kuwa ni ile hali ya kuifanya akili yako kuto kuona kuwezekana kwa jambo kwa kila kitu, yaani hapa wewe umejiwekea mipaka kwa kuitawaza akili yako na neno haiwezekani, ndio maana kila jambo ambalo unakuwa ukitaka kulifanya wewe unaona ni kama haliwezekani, hata kama linawezekana. Sasa jambo hili ndilo limekuwa likikurudisha nyuma na kukufanya ubaki pale pale kwa kuwa akili yako imejaa neno haiwezekani haiwezekani na huu ni mpaka ambao umekuwa ukiwatesa watu wengi sana na kuwafanya waanze kuwaona baadhi ya watu kama wenye bahati, kubalikiwa, waajabu kuliko wao kumbe tatizo sio bahati au kubalikiwa tatizo ni mipaka wanayojiwekea wenyewe. Maana hao unaowaona ni kama wana bahati na wamebalikiwa hawajajiwekea mipaka ya haiwezekani bali wao huona fursa na wakaitumia fursa husika moja kwa moja huku wakiamini kuwa jambo fulani lawezekana hata kama litachukua muda au litawapitisha katika magumu gani kimaisha wao ambacho hutazama ni kutaka kuona kuwa wanachokitaka kimetimia.

Mpaka mwingine ni ile hali ya ngoja ngoja, yaani umeyajaza maisha yako na ngoja ngoja tena wakati mwingine umekuwa ukiendelea kuihararisha hiyo ngoja ngoja yako kwa methali na misemo kama vile, “polepole ndio mwendo”, “haraka haraka haina Baraka”, “mwenda pole hajikwai”, “subira yavuta heri” n.k. kwa kuwa umetawaliwa na ngoja ngoja nyingi hivyo umekuwa mzito wa kufanya maamuzi hata kwa jambo ambalo linatakiwa kuchukuliwa hatua za haraka na hii imekupelekea sasa ushindwe kufanikiwa maana umekuwa na nyingi ngoja ngoja kuliko vitendo halisi. Sina maana kuwa ukurupuke sasa na uanaze kupalamia kila unachokiona hapana nachotaka hapa ni wewe kuifanya akili yako ichemke na iweze kufanya upembuzi yakinifu haraka haraka ndani ya muda mchache na uweze kuwa umepata majibu fasaha.

Mpaka wa mwisho ni kutokukubali mabadiliko, kuna watu huwa wanapenda kwenda kinyume na wakati au nyakati, yaani wao huwa wanataka kubaki pale pale hata kama kuna mabadiliko yalishatokea na mifumo ya vitu imebadilika lakini wao hutaka kubaki pale pale kwa misemo yao ya “old is Gold”. Sasa kuwa makini sana maana dunia inabadilika sana kila siku kama utabaki pale pale hii inaaama hautafanikiwa na kusonaga mbele.

Hiyo ni mipaka michache ambayo umekuwa ukiiweka katika akili yako na inakurudisha nyuma. Anza kuitoa sasa.


Makala hii imeandikwa na Baraka Maganga, waweza kuwasiliana na mwandishi wa makala hii kwa nambari ya simu 0754612413 au kwa barua pepe bmaganga22@gmail.com


Sehemu Nne Za Kuzishughulikia Ipasavyo Ili Kuwa Mwenye Mafanikio.

Image result for four pillars
Mafanikio ni kanuni, na kanuni hizi ndizo zinazokuongoza kuwa kipi ufanye na kipi usifanye. Katika maisha yetu wengi wetu tumekuwa tukipata shida sana ya kuwa ni jambo gani tunatakiwa kufanya au ni mambo gani tunatakiwa kufanya ili kuweza kuyapata mafanikio na ni jambo gani hatutakiwi kufanya ili kuepuka kuto kuwa na mafanikio. Kiujumla mimi huwa naamini kuwa mafanikio huwa yanatokana na kujua nini unapaswa kufanya na wala haihusiani na bahati wala nini. Karibu tujifunze kwa pamoja mambo manne ya kuzingatia ili kuweza kuyapata mafanikio.

1.   Afya.
Afya ni kitu cha muhimu sana kwa maisha ya binadamu, hili ni jambo ambalo liko wazi kwa kila mtu lakini pamoja na uwazi huu ni wachache sana wanaozingaatia swala la afya zao. Afya ni muhimu kwa kuwa ndio inatufanya tuweze kwenda katika maeneo yetu ya kazi, ndio inayotufanya tuweze kupanga na kutekeleza mipango yetu. Jiulize swali rahisi tu ukiwa mgonjwa unaweza kwenda kazini au katika biashara yako?, nafikiri jibu ni hapana sasa kama hauwezi basi tambua kuwa afya yako ni kitu cha muhimu sana katika mafanikio yako. Hivyo jitaidi kuimarisha afya yako kwa kutokula vyakula ambavyo sio rafiki wa mwili wako, fanya mazoezi na fuata kanuni zingine za kiafya.

2.   Akili.
Hapa katika swala la akili sina maana kuwa uende hospitali na kwenda kupima akili yako kama ipo sawa au la, hapana hapa nachotaka ni kitu kimoja tu kuwa makini na chakula unachoirisha akili yako. Yaani hapa usiipe akili yako taarifa hasi, usiiweke akili yako iwe ipo ipo tu bila kuipa changamoto yoyote ile, ifanye akili yako iwe inachemka muda mwingi, na hili utaweza kulifanya kama tu utaamua kuanza kusoma vitabu, kuhudhuria semina, na kufuatilia taarifa zinazokuhusu. Kwanini akili kinakuwa kipengele moja wapo cha kuzingatia katika makala yetu ni kwasababu moja tu, akili ndio msingi wa mafanikio yako yaani kama akili yako inachemka basi ni dhahiri utayapata mafanikio na kama akili yako haichemki basi huwezi kuyapata mafanikio, na uwezo wa kuichemsha akili upo mikononi mwako hivyo fanya kuichemsha sasa.

3.   Imani.
Kila mtu amekuwa na kitu anachokiamini katika maisha yake, lakini mimi hapa nataka kukueleza kitu kimoja tu juu ya imani. Ni kwamba mafanikio yanaendana sana na imani yako, hii ni kumaanisha kuwa wewe unaamini nini katika yale unayoyafanya kama unaamini utafanikiwa basi ni dhahiri kuwa itakuwa hivyo. Na jambo la mwisho nalotaka kukuweka wazi juu ya imani ni kwamba hakuna imani nusu, yaani unakuwa hueleweki eleweki, hapa nachosema imani yako lazima iwe upande fulani kama ni kuamini kuwa utafanikiwa basi iwe hivyo na kama ni kuamini kuwa utashindwa basi iwe hivyo. Usiwe mtu wa sijui ntafanikiwa au sitafanikiwa au mtu wa lakini naweza au siwezi.

4.   Mahusiano.
Hapa nazungumzia mahusiano yako na watu wanaokuzunguka, kumbuka kuwa sio lazima uongee au uwasiliane na kila mtu ila ni muhimu ukawa na mahusiano mazuri na jamii yako inayokuzunguka hii itakusaidia sana katika hata kuweza kupata wateja katika biashara yako, kupata taarifa muhimu juu ya fursa ambazo hata ulikuwa huzijui. Hivyo jenga mahusiano yako vyema na watu. Kumbuka hakuna mtu anaefanikiwa kwa kuwa na mahusiano mabovu na wengine.

Makala hii imeandikwa na Baraka Maganga, waweza kuwasiliana na mwandishi wa makala hii kwa nambari ya simu 0754612413 au kwa barua pepe bmaganga22@gmail.com


Mambo Matatu (3) Ambayo Ni Kinyume Na Mafanikio.

Image result for anti clockwise
Kila wakati umekuwa ukitaka ufanikiwe, umekuwa ukitaka uonekane ni mwenye mafanikio ili pengine uweze kuwa msaada kwa wadogo zako, ndugu zako, wazazi na hata jamii inayokuzunguka. Lakini kinachokuja kutokea huwa ni kinyume na yale uliyoyapanga kwani umekuwa huyapati hashwa yale mafanikio ambayo umekuwa ukiyahitaji kwa muda. Sababu za kukufanya uwe hivyo zaweza kuwa nyingi mno, na hii ni kutokana na sababu kuwa mafanikio ni mchakato ambao una hatua zake muhimu ambazo unatakiwa kuzifuata. Mafanikio yana kanuni zake ambazo sharti uzifuate na uzisimamie bila kufanya hivyo ni dhahiri kuwa huwezi kupiga hatua yoyote ile katika maisha yako. Sasa sababu moja wapo ya kukufanya usifanikiwe mpaka leo ni kwa kuwa unakwenda kinyume na mafanikio, yaani upo kinyume na mafanikio kwa kuwa unafanya mambo ambayo hayawezi kukuletea mafanikio hata siku moja mambo hayo yaweza kuwa mengi lakini hapa nimekuwekea mambo matatu tu ambayo ni haya hapa:-

1.   Kujifariji
Katika maisha yetu binadamu tumekuwa ni watu wenye kupenda sana kujifariji au kufarijiwa, hii ni kutokana na kuwa kuna wakati huwa tunapitia magumu mfano msiba, hapa ni muhimu mtu afarijiwe au kujifariji. Lakini mimi sizungumzi huko nacho kizungumzia mimi ni katika kuyasaka mafanikio, ambako huko ndiko tumekuwa tukijifariji sana na haswa kwa misemo mingi kama vile kama:- kama ipo ipo tu, haikuwa bahati yangu, ipo siku yangu, muda bado, haikuwa fungu langu n.k. maneno yako yote ni sawa na sahihi kabisa lakini mimi nakuambia kuwa huku ni kujifariji tu maana, utakuta mtu umeshindwa kuweka juhudi za kutosha katika lile ulilokuwa unalifanya, matokeo yake umeshindwa na hapo sasa ndipo unaanza kujifariji na hio misemo yako. Naomba nikuambie kuwa kujifariji unakokufanya ni kinyume na mafanikio na kama ukiendelea hivyo basi tambua kuwa mafanikio kwako itakuwa hadithi. Maana kujifariji kutakufanya uone kama vile unaonewa na hali ikisha kuwa hivi basi na akili yako itaduma na kuacha kufanya kazi kwa kuwa tu umehisi unaonewa.

2.   Utumwa.
Swala la utumwa ni pana kidogo, hii ni kutokana na sababu kuwa utumwa waweza kugawanyika katika sehemu nyingi, lakini mimi hapa nitaugawa utumwa katika makundi mawili ambayo ni utumwa wa vitu, na utumwa kwa watu/mtu. Kuna watu ni watumwa wa watu wengine yaani hawa ni wale ambao hawawezi kufanya jambo fulani pasipo mtu fulani. Yaani wao wapo wapo tu hawawezi kujifanyia maamuzi pasipo kuwepo na mtu fulani, mfano utakuta mtu anawategemea wazazi au ndugu kama vile kaka au dada ndio wamfanyie maamuzi katika maisha yake. Hii ni kinyume na mafanikio kwani mafanikio yanahitaji wewe ufanye maamuzi juu ya maisha yako. Utumwa wa vitu ni ule wa kupenda au kutaka kuwa na kitu kiasi kwamba kile kitu kinakutawala na huwezi kufanya mambo ya msingi. Hivyo basi utumwa wa vitu na watu/mtu ni kinyume na mafanikio. Kwa kuwa binadamu kwa asili yake ni mtawala wa vitu na sio mtawaliwa wa vitu.

3.   Uongo.
Jambo hili pia ni kinyume cha mafanikio kwa maana kuwa mafanikio hayahitaji ujanja ujanja au kuficha ficha mambo bali mafanikio yanahitaji uwe mkweli. Mtu muongo anaweza kujidanganya mwenyewe kwa kufanya mambo ambayo sio au anaweza kuwadanganya wengine na uongo wa kuwadanganya watu wengine ni kitu hatari sana kwa kuwa watu wanapenda kushirikiana na watu wakweli sasa wakigundua wewe ni muongo hawawezi kufanya shughuli yoyote na wewe, iwe biashara, kikundi cha kusaidiana, kazi n.k. hivyo epukana na uongo kama kweli unataka kufanikiwa maana uongo ni kinyume na mafanikio.

Makala hii imeandikwa na Baraka Maganga, waweza kuwasiliana na mwandishi wa makala hii kwa nambari ya simu 0754612413 au kwa barua pepe bmaganga22@gmail.com


Leo Ndio Siku Ya Mwisho Ya Kupata Kipato Cha Ziada Mtandaoni Kwa Kutumia Blog.

Habari rafiki, mara baada ya kupeana taarifa kwa takribani siku kadha wa kadha kuhusiana na semina ya pata kipato cha ziada mtandaoni kwa kutumia blog. Tunapenda kuchukua nafasi hii kukufahamisha kwamba leo siku ya ijumaa ya tarehe 13/01/2017 ndio siku ya mwisho kwa wewe ya kupata nafasi ya kujiunga na semina hii ya pata kipato cha ziada mtandaoni kwa kutumia blog. Kwa hiyo, ni muhimu ukachukua hatua kwa kujiunga nasi mapema kabla ya siku hii ya leo kuisha. Kwani kama tulivyosema hapo awali kuwa mara baada semina hii kumalizika basi haitokuja kurudiwa tena. Yaani semina hii itaendeshwa kwa mara moja tu na haitokuja kurudiwa tena.

Ndugu rafiki, kupitia semina hii muhimu na ya kipekee utakwenda kujifunza jinsi ya kupata kipato cha ziada mtandaoni kwa kutumia blog yako. Semina hii ya pata kipato cha ziada mtandaoni kwa kutumia  blog itaanza siku ya jumatatu ya wiki ijayo ya tarehe 16/01/2017 hadi tarehe 28/01/2017, na semina hii itakwenda kufanyika kwa njia mtandao ( barua pepe). Na kwa wale ambao kwao ndiyo mara ya kwanza kupata taarifa kuhusiana na semina hii wanaweza kufungua maandishi haya (Pata kipato cha ziada mtandaoni kwa kutumia blog) kwa kusoma makala hiyo ili waweze kupata taarifa zaidi kuhusiana na mafunzo hayo.


Kujiunga na semina hii ya PATA KIPATO CHA ZIADA MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG tuma ada  yako ambayo ni elfu kumi na tano (15,000/=) kwa M-PESA ( 0767382324) Au kwa Tigo pesa ( 0675555987). Na kisha mara baada ya kutuma ada yako hakikisha unatuma pia na e-mail  yako kwa meseji kwenye mojawapo kati ya namba hizo ili tuweze kukuunganisha. Tunakutakia utekelezaji mwema na tupo pamoja.

Changamoto (4) Nne Zinazokutoa Katika Mstari Wa Mafanikio.

Image result for challenges
Changamoto ni kitu ambacho ni cha kawaida sana kwa mtu ambae anayasaka mafanikio, hili huwa linatambulika kwa watu walio wengi pindi wanapojiingiza katika safari hii ya kuyasaka mafanikio lakini watu hawa huwa wanakumbwa na tatizo moja kuwa pindi wapatapo au kukabiliwa na changamoto hizi huwa hawana uwezo wa kuzitatua na kusonga mbele.changamoto tunaweza kuzigawa katika changamoto za mazingira yaani zile za asili na changamoto zile ambazo tunazitengeneza wenyewe. Sasa hapa nakuletea changamoto nne tu ambazo huwa tunajitengenezea na  zinatusumbua tulio wengi.

1.   Kutafuta sababu ndani ya watu, hii ni changamoto ambayo huwa inatukabili watu tulio wengi sana. Hii changamoto iko hivi yaani unapata tatizo au shida fulani au unashindwa kufanya kitu fulani, badala ya kujitathimi wewe kama wewe kwanini umeshindwa unaanza kutafuta nani aliyesababisha ushindwe. Hii haiwezi kukusaidia kwa sababu hapa ni sawa na unatafuta nani wa kumlaumu. Hivyo sikushauri kutafuta sababu ndani ya watu.

2.   Kutokujitathimini, hapa ni kuwa tumekuwa tukiishi tu bila kujali tunaishi vipi na wala tunataka tuende wapi katika maisha yetu. Hii ni kwasababu hatuna muda wa kukaa na kutathimini maisha yetu tuyapeleke vipi bali tunaishi tu ilimradi tumeamka basi maisha yanaendelea, kwako wewe unaetaka kufanikiwa na kutaka kufika mbali kimaisha basi hakikisha unaweka utaratibu wa kujitathimini kila baada ya muda fulani yaweza kuwa wiki, mwezi au hata kila siku unafanya tathimini ya siku. Yaani kila siku unafanya tathimini kipi umepanga siku hiyo na kimeendaje hii itakusaidia kupata mwendelezo na mwelekeo mzuri wa maisha.


3.   Kutokujipa mitihani, maishani haswa kwa watanzania tulio wengi tumekuwa na mazoea ya kuwa tunafanya mitihani shuleni tu na baada ya hapo hatufanyi tena. Kuna mtu alimaliza shule mwaka 2000 huko mpaka leo hajawahi fanya mtihani tena, jiulize wewe mara ya mwisho umefanya mtihani lini?. Tena mtihani wa kupewa wa kujipa je?, sasa nataka leo ufanye jambo moja kuwa anza kujipa mitihani, hapa sitaki uanze kujipa mitihani kama vile shuleni, hapana hapa mitihani yako iwe ni katika kuyatekeleza majukumu yako. Mfano umejiwekea malengo ya miezi mitatu uwe umefanya jambo fulani, sasa anza kujipa mtihani kwamba ili niweze kutimiza lengo hili ndani ya wiki hii niwe nimefanya jambo fulani sasa huo ndio mtihani unaojipa, kwahiyo ndani ya wiki utakuwa unafanya huo mtihani wako na matokeo yake utayapata katika kujitathimini. Ndio maana nikakuambia katika changamoto ya pili kuwa jifanyie tathimini ila huwezi kufanya tathimini bila kuwa na mtihani uliojipa.

4.   Ufuatiliaji mbovu, kama kuna kitu kinatusumbua watanzania basi ni pamoja na ufuatiliaji, tumekuwa ni wafuatiliaji wabovu sana na hii imetufanya tuanze kujijengea mazingira ya kutumikishwa maana hatuwezi kufanya jambo fulani bila ya kusimamiwa au kuambiwa na mtu fulani. Sasa kwako wewe unaetaka mafanikio kuwa mfuatiliaji wa maisha yako kwa vitendo zaidi kuliko maneno. Kama unamradi wako fika mahali ulipo simamia mwenyewe na sio uwe mpiga simu tu kila siku.

Kumbuka hizi changamoto sio za kimazingira bali ni zile za kutengenezwa na binadamu yaani binadamu sisi kama sisi ndio tumekuwa tukizitengeneza,sasa swala la kujiuliza ni kuwa utaendelea kujitengenezea changamoto hizi au utaacha. Kumbuka kama huta acha huwezi kufanikiwa.

Makala hii imeandikwa na Baraka Maganga, waweza kuwasiliana na mwandishi wa makala hii kwa nambari ya simu 0754612413 au kwa barua pepe bmaganga22@gmail.com


Mara Zote Huonekana Haliwezekani Mpaka Lifanikiwe.

Jitihada kubwa katika maandalizi zilifanyika ili kumwezesha Roger Bannister akimbie maili nzima kwa muda wa pungufu ya dakika nne. Roger Bannister alikuwa na mazoezi ya kudumu yaliyohusisha shughuli ngumu ya kupanda milima. Ndipo ulipotokea ushindi mnono uliosababisha macho yote ulimwenguni kote yaelekezwe kushuhudia tuzo aliyotunikiwa kijana huyo mpenzi wa riadha. Ilikuwa ni asubuhi njema hapo mei 6, 1954, siku ambayo Roger Bannister alikuwa akiisubiri kwa hamu kubwa sana huku akijiandaa kimwili, kiakili, na kihisia kwa takribani miaka kadha wa kadha. Naam, na siku moja kabla ya tarehe hii muhimu,  Roger Bannister aliteleza sakafuni akawa anachechemea!!. Hata hivyo kesho yake alijiunga katika mbio za riadha,  naye Roger Bannister akamaliza maili moja kwa dakika 3 sekunde 59.4  ( 3:59.4), na akawa ndiye mtu wa kwanza hapa duniani kuweza kumaliza mbio za maili moja kwa muda pungufu ya dakika nne!. NI maajabu yaliyoje rafiki!.

Hili lilikuwa ni moja ya tukio kubwa sana na la kipekee  lililoushangaza ulimwengu, kwani kabla ya hapo tafiti kadhaa zilikwishafanywa na madaktari zikibainisha kwamba, ni jambo lisilowezekana kamwe kwa binadamu kuweza kukimbia mbio za maili moja kwa muda pungufu ya dakika nne. Yaani iliaminika kwamba hilo ni jambo lisilowezekana kabisa na ni hatari sana kwa maisha ya binadamu. Imani hiyo ya kuamini kwamba kamwe binadamu hatoweza kuja kukimbia mbio za maili moja kwa muda pungufu ya dakika nne iliaminiwa na kushikiliwa na wengi  ingawa haikuwa na ukweli wowote ndani yake. Na imani hii ikaja kutupiliwa mbali wakati ambapo Roger Bannister alipoweza kukimbia maili moja kwa muda pungufu ya dakika nne. Na imani hiyo ikazidi kutupiliwa mbali zaidi na zaidi wakati ambapo mwanariadha mwingine raia wa Austaria aitwaye John Landy, alipoweza kuivunja rekodi ya Roger Bannister kwa  kukimbia maili moja kwa muda pungufu ya dakika  tatu. John Landy aliivunja rekodi ya Roger Bannister siku 46 tu baadaye mara baada ya Bwana Roger Bannister kuweka rekodi yake.

Na hapo baadaye walipokutana wenyewe kwa wenyewe bwana Roger Bannister na John Landy. Wote kwa pamoja wakaweka rekodi nyingine kwa kuweza kukimbia mbio za maili moja kwa dakika 3 sekunde 43:13. Ni maajabu yaliyoje rafiki?, Kwani hili ni jambo ambalo kwa zaidi ya miongo kadhaa iliyopita lilikuwa likiaminika na kusemekana kwamba ni jambo lisilowezekana kamwe. Lakini kwa sasa tunaweza kuona watu wakiweka rekodi baada ya rekodi na kisha zinavunjwa. Kumbe  kisichowezekana kinawezekana.  Raisi  wa zamani wa Afrika kusini ambaye kwa sasa hatunaye tena hapa duniani bwana Nelson Mandela aliwahi kusema “mara zote huonekana haliwezekani mpaka lifanikiwe”.

Ni lini ulifanya kisichowezekana?
Ndugu rafiki, Hivi mara ya mwisho kwa wewe kufanya kile kisichowezekana ilikuwa ni lini? Ni lini uliacha kujaribu kufanya jambo fulani sababu watu wengine, ndugu, rafiki, na hata jamaa zako walikwambia kwamba hilo unalotaka kulifanya kamwe halitowezekana?. Kuna maelfu ya mambo kadha wa kadha katika maisha yako ya kila siku ambayo mpaka sasa bado hujayapa nafasi ya kuyafanya kutokana na kuamini kwamba hayatowezekana. Mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine ndiyo yangelileta tofauti kubwa sana katika maisha yako na kwa wengine.

Ndugu rafiki, ukweli ulio wazi ni kwamba katika maisha kila jambo linawezekana, yaani hakuna kile kisichowezekana chini ya jua. Unachotakiwa wewe ni kuwa na imani juu ya uwezo wako, juu ya kile unachokitaka, kujitoa kwa dhati pamoja na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kuelekea kwenye utimilifu wa ndoto na malengo yako uliyojiwekea.

Penye Nia Ndipo Penye Njia.
Kuna msemo unaosema “penye nia ya dhati ndipo penye njia”. Tambua kwamba, pale penye nia ya dhati ndipo penye njia ya kweli. Kamwe usikate tamaa, amini na ishi ndoto zako kwani kila jambo chini ya jua linawezekana. Usikae tu na kulalamika kwa kushindwa kwako kufanikisha hili na lile. Kwani kulalamika  pekee hakutoweza kuyafanya maisha yako kuwa bora bali utakuwa unaongeza tatizo juu ya tatizo, sababu pale unapolalamika unakuwa unamaanisha kwamba wewe hauna uwezo wala nguvu ya kutatua matatizo yako, jambo ambalo ni hatari sana kwani safari ya mafanikio katika maisha huwa inaanza kwa kushika hatamu juu ya maisha yako . Usikae tu na kusema kwamba unataka hiki na kile bali chukua hatua sasa na usiwe mwoga wa kujaribu mambo mapya kwa hofu ya kuja  kushindwa, kukataliwa, kuchekwa, na hata kukosolewa pia. kwani huko kwenye kushindwa na kufanya makosa ndiko sehemu sahihi kwa wewe kujifunza. Kwa hiyo chukua hatua sasa katika kuelekea kwenye malengo na ndoto zako, kwani mpaka sasa tayari una rasilimali zote muhimu unazopaswa kuwa nazo ili kuweza kufanikisha ndoto na malengo yako katika maisha. Na ninaposema kwamba tayari una rasilimali zote muhimu unazopaswa kuwa nazo, huwa nina maana kwamba tayari una mitaji mitatu muhimu na ya kipekee ambayo ni watu, akili , na muda.

Ota Ndoto Kubwa.
Na unapoamua kuwa tofauti na wengine katika maisha. Unapoamua kuwa na ndoto kubwa katika maisha, basi tarajia ama tegemea kukumbana na vikwazo vya kila aina pamoja na kukatishwa tamaa. Ni lazima utakumbana na changamoto na vikwazo vyenye lengo la kuona ukishindwa kufanikisha ndoto na malengo yako uliyojiwekea katika maisha. Ni lazima pia utakutana na watu watakaokukatisha tamaa kwa kukwambia hilo unalotaka kulifanya kamwe halitowezekana. Na sababu kubwa ya wengi kukwambia kwamba hilo unalolitaka kulifanya halitowezekana, ni kutokana na fikra hasi za kushindwa walizonazo wengi kwa kushikilia picha na mawazo ya neno” haiwezekani” . Ndugu rafiki, kamwe usitishwe na hali hiyo bali unatakiwa utambue kwamba, changamoto na vikwazo vimewekwa katika maisha na katika safari yetu ya mafanikio ili kwa pamoja viweze kutujaribu kwa kutaka kujua ni kwa kiasi gani hasa tumejitoa katika kupata kile tunachokitaka. Na kadri tutakavyozidi kuwa wavumilivu na ving’ang’anizi kwa kuendelea kushikamana na ndoto na malengo yetu tuliyojiwekea, ndivyo navyo vikwazo na changamoto vitakavyozidi kupungua. Changamoto na vikwazo hutusaidia sana katika kutukomaza kiakili na kihisia. Na hilo ni hitaji muhimu ambalo kila mtu anapaswa kuwa nalo ikiwa anataka kufanikiwa, yaani ukomavu wa kihisia.

Ishi ndoto zako. Amini kila jambo linawezekana. Ondoa neno “siwezi” au “ haiwezekani” akilini mwako. Kwani mawazo ya aina hiyo wala si yako. Kwani ulikuja hapa duniani kupitia wazazi wako ukiwa na nuru kubwa ndani yako inayoamini kwamba kila jambo linawezekana.  Lakini kadri ulivyozidi kukua ndivyo nuru yako nayo ilivyozidi kufifia kutokana na ushawishi mkubwa uliokumbana nao kutoka kwenye mazingira uliyokulia. Wakati ungali mtoto mchanga hukuwa unajua kwamba jambo fulani haliwezekani lakini ulipozidi kuwa kijana ndivyo ukaanza kusikia na kuamini maneno kadha wa kadha kama vile “ ili jambo kamwe  haliwezekani”, “ kamwe huwezi “ ,“ wewe si lolote si chochote” na kadhalika kutoka kwa marafiki, ndugu, na hata jamii yako kwa ujumla.

Ndugu rafiki, Ota ndoto kubwa, ishi ndoto yako na amini kwamba kila jambo linawezekana. Na kama unashindwa kuamini hilo basi tazama hapo nyuma kwa kuangalia na kufuatilia historia za watu wengi walioweza kufanya mambo makubwa, mambo ambayo yalisemekana hapo kabla kuwa hayatowezekana ila yakawezekana. Watazame watu kama kina Roger bannister,  steve job (mgunduzi wa taa ya meme), Orvile na Wilbur Wright (wagunduzi wa ndege), na hata helen keller (huyu alikuwa kipofu na kiziwi lakini aliweza kufanikisha mambo makubwa).

Rafiki yangu, Kitu kimoja kinachowatofautisha watu waliofanikiwa na wasiofanikiwa ni zile ndoto walizonazo maishani, watu waliofanikiwa huwaza ndoto kubwa na hii huwawezesha kutumia nguvu, muda, juhudi na maarifa kwa muda mrefu ili kutimiza ndoto na malengo waliyojiwekea. Achana na ndoto ndogo ndogo na waza mambo makubwa. Chochote kile anachoamini mwanadamu ni lazima  atakifanikisha kwani hakuna linaloshindikana. Jifunze kuutumia vizuri ubongo wako ili ukufanikishe. Kwani ubongo wako ni sawa na ardhi yenye rutuba inayotegemea unapanda nini kichwani mwako. Kama utapanda mbegu nzuri basi utapata matokeo mazuri. Waza mambo makubwa, kuwa na fikra chanya na amini kila jambo linawezekana.

Hapo kabla wengi waliamini kwamba kamwe hatutapaa angani lakini Orvile and Wilbur Wright wakaamini inawezekana. Thomas Edson alikuwa na ndoto kubwa kwamba ipo siku binadamu  atatumia taa ya umeme, na baada ya miaka zaidi ya kumi ya majaribio na kushindwa zaidi ya mara 999 lakini mara ya 1000  akafanikisha ndoto yake. Ndugu rafiki amini kila jambo linawezekana. Na mtu yeyote akikwambia kwamba hilo unalotaka kulifanya halitowezekana basi tambua kwamba hiyo ni ishara ya kuwezekana kwake. Nakutakia utekelezaji mwema.

MUHIMU

Semina hii ya PATA KIPATO CHA ZIADA MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG itakayofanyika kwa njia ya mtandao itaanza Jumatatu ya wiki ijayo ya tarehe 16/01/2017 hadi tarehe  28/01/2017.Kupitia semina hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza kipato cha ziada mtandaoni kwa kutumia blog. Kwa taarifa zaidi kuhusiana na semina hii bonyeza maandishi haya ( SEMINA : Pata Kipato Cha Ziada mtandaoni kwa kutumia blog). Na gharama ya semina hii ni tsh elfu kumi na tano ( 15,000). Na mwisho wa kufanya malipo kwa ajiri ya kujiunga na mafunzo hayo ni Ijumaa ya wiki hii ya tarehe 13/01/2017. Na kufanya malipo ili kujiunga na mafunzo haya muhimu na ya kipekee utalipia ada yako moja kwa  moja kwa kutumia mojawapo kati ya namba zifuatazo ; M-PESA ( 0767382324) Au TIGO PESA ( 0675555987). Na ukishalipia ada yako utatuma na e-mail yako pia kwa meseji kwenye mojawapo ya namba hizo ili tuweze kukuunganisha na mafunzo hayo. 

Funguo Mbili Za Mafanikio Yako Mwaka Huu.

Image result for keys
Umekuwa ukipigana na kupambana vikali sana kwa miaka kadhaa iliyopita huko nyuma, pengine umekuwa ukipata wastani kuliko ulivyotarajia, pengine umekuwa ukipata kidogo kuliko ulivyokuwa umepanga, na pengine umekuwa haupati kitu kabisa. Je unashangaa hali hii?, kama unashangaa mimi hapa nataka uachane na mshangao huo na badala yake mwaka huu uwe ni mwaka wa mafanikio makubwa kwako mwaka ambao utakwenda kutimiza yale ambayo umeshindwa kuyatimiza kwa miaka mingi sana huko nyuma. Kumbuka makala hii haijabeba muujiza ila imebebe funguo mbili tu za mafanikio yako ambazo ukizifuata basi mafanikio yako utayaona mwaka huu.

Kama umekuwa hupati matokeo ambayo umekuwa ukiyatarajia basi tambua kuwa kuna mahali ambapo umekuwa ukipakosea yaani kuna mahali hauendi sawa sasa leo sikutajii unapokosea ila nakupa funguo mbili tu za kukuwezesha wewe kuweza kufanikiwa mwaka huu. Funguo hizo ni hizi zifuatazo:-

1.   Imani, kama kuna kitu cha kwanza katika mafanikio basi ni imani. Waandishi wengi wamekuwa wakiandika kuwa ukitaka kufanikiwa weka malengo yaani wengi wameweka malengo kama kitu cha kwanza, sipo hapa kuwapinga wala kuwakosoa au kusema ni wazushi ama namna gani hapana nachotaka kusema hapa ni kuwa tanguliza imani kwanza. Maana pasipo imani tambua kuwa hata hayo malengo huwezi kuyatekeleza maana kupitia imani ndipo unapopata msukumo hata wa kuweka malengo na kuamini kuwa utakwenda kuyatekeleza kama ulivyo yapanga.

Imani ni jambo ambalo limesisitizwa hata katika vitabu vya dini yaani lazima uwe na imani katika au juu ya jambo unalo lifanya au utakalokwenda kulifanya. Mfano wapo watu wengi sana wanaoyataka mafanikio lakini hawaamini kuwa wanaweza kufanikiwa. Sasa sitaki leo hii na wewe uendelee kufanya kosa juu ya kosa anza kuwa na imani juu ya yale unayoyafanya hata kana utapigwa na kukataliwa kwa namna gani amini kuwa utafanikisha jambo fulani hata kama watu watakuambia haliwezekani kwa namna ipi. weka weka imani juu yako na mambo yako.

2.   Jiamini, kama kuna swala ambalo linawasumbua vijana wengi kwa sasa basi ni swala la kujiamini. Vijana wengi sana hawajiamini na ndio maana wamekuwa wanafanya mambo ambayo hata hayaeleweki yaani ukiwaangalia utaona kuwa wanamapungufu katika kujiamini kwao. Maana utakuta kijana hana hata uwezo wa kujielezea kuwa yeye ni nani, anataka nini, anatoka wapi na anataka kwenda wapi?. Sitanii mambo haya yapo miongoni mwetu. Mara ngapi umekuwa ukishuhudia watu wanakosa cha kuongea mbele za watu pindi wanapotakiwa kufanya hivyo?.

Nataka ujiulize leo kama hujiamini kiasi kwamba huna uwezo wa kujielezea kwa watu lakini una wazo la kuja kuwa mfanyabiashara, utafanyaje biashara husika ikiwa huna uwezo wa kuongea na watu yaani kujielezea mbele za watu huwezi. Utaipigia vipi debe bidhaa yako husika?, utawasilisha vipi bidhaa yako mbele za watu ikiwa hujiamini. Muda mwingine kujiamini huwa kunatokana na kukosa maarifa juu ya jambo fulani hivyo basi hakikisha leo hii unapata maarifa juu ya jambo unalolifanya ili tu uweze kufanikisha mambo yako. Ni wengi sana tumekuwa tukipoteza nafasi kisa tu hatujiamini, sasa jitathimini leo hii na uone unajiamini vipi, kama hujiamini basi tambua kuwa hiyo ni sababu ya kwanini ulikuwa hufanikiwi hapo nyuma na je unataka hali hii iendelee kukukumba?.


Makala hii imeandikwa na Baraka Maganga, waweza kuwasiliana na mwandishi wa makala hii kwa nambari ya simu 0754612413 au kwa barua pepe bmaganga22@gmail.com